IQNA

Rais Hassan Rouhani wa Iran

Nchi kusimamiwa bila kutegemea pato la mafuta ni dhihiriso la uwezo wa Iran katika vita vya kiuchumi

20:47 - July 14, 2020
Habari ID: 3472961
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kuendesha nchi hii bila ya kutegemea sana pato la mauzo ya mafuta ni kielelezo cha nguvu kubwa ya Iran katika medani ya vita vya kiuchumi.

Rais Rouhani ambaye leo alikuwa akihutubia kikao cha Kamati ya Uratibu wa Masuala ya Uchumi cha baraza la mawaziri amesema kuwa, Wamarekani walidhani kwamba ustawi wa kiuchumi wa Iran ungesimama baada ya kuanzisha vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, lakini hii leo nchi hii inaendeshwa kwa mipango mizuri bila ya kutegemea pato la mafuta, na huu ni ushindi mkubwa wa taifa la Iran katika vita vya kiuchumi. 

Vilevile ameashiria athari mbaya za maambukizi ya virusi vya corona katika hali ya kiuchumi ya nchi mbalimbali duniani na kusema kuwa: Katika mazingira haya ambamo hata nchi zilizoendelea zinakabiliwa na matatizo katika kudhamini mahitaji ya kila siku ya wananchi, Iran imevuka vyema kipindi hicho kwa tadbiri, kazi nzuri ya asasi mbalimbali na ushirikiano mwema wa wananchi. 

Takwimu za karibuni za Wizara ya Afya ya Iran zinaonyesha kuwa, zaidi ya Wairani laki mbili 62 elfu na 173 wameambukizwa virusi vya corona na laki mbili 25 elfu na 270 wamepona ugonjwa huo.  

3910501

captcha