IQNA

Kampeni katika Twitter kupinga kitendo cha Google kufuta Palestina katika ramani ya dunia

19:15 - July 17, 2020
Habari ID: 3472970
TEHRAN (IQNA) - Shirika la intaneti la Google limekosolewa vikali watumiaji wa mitandao mbali mbali ya kijamii baada ya kuiondoa "Palestina" katika ramani zake za dunia, na badala yake kupachika jina la "Israel."

Maelfu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ndani na nje ya Palestina wameghadhabishwa mno na kitendo hicho cha shirika la Google, na wametumia hashtagi za #IacheHuruPalestina na #SimamaNaPalestina kulikashifu na kulishutumu vikali shirika hilo la Kimarekani kwa hatua yake hiyo ya kichokozi na kichochezi.

Mmoja wa watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwa jina Syed Hashima, ameandika katika ukurasa wake wa mtandao huo wa kijamii kuwa: Mnaweza kuiondoa (Palestina) katika ramani, lakini hamuwezi kufuta historia yao na machungu yao. Palestina tu ndiyo nchi tunayoitambua.

Naye Muhammad Abbas ameandika: Ramani za Google na Apple zimeiondoa Palestina katika ramani za dunia. Kwa mujibu wa Google, hivi sasa hakuna pahala panapotambulika kama Palestina. Mauaji ya kimbari, wizi wa ardhi na njama za kishirika, yote haya yanafanyika kwa jina la Israel. #IacheHuruPalestina.

Shirika hilo la Kimarekani lilichukua hatua hiyo ya kifidhuli Jumanne iliyopita, ambapo mbali na kuondoa neno Palestina katika ramani zake zote za dunia, lakini pia limeyaarifisha maeneo mawili ya Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, kama sehemu za Israel.

Huko nyuma pia, Wizara ya Utalii ya utawala wa Kizayuni wa Israel imewahi kuchapisha ramani mpya ya mji wa Quds tukufu ambayo ndani yake maeneo yote matakatifu ya Kiislamu na Kikristo yamefutwa. Wapalestina wanasisitiza kuwa, vitendo hivyo vya Wazayuni na Wamarekani vinakusudia kuyayahudisha maeneo matukufu ya dini za Kiislamu na Kikristo yenye historia ndefu sambamba na kupotosha utambulisho wa maeneo hayo.

3910907/

captcha