IQNA

13:31 - August 07, 2020
Habari ID: 3473042
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetoa wito wa kuanzishwa kamati ya mirengo yote ya Palestina kwa ajili ya kuutetea mji wa Quds Tukufu (Jerusalem) na kuulinda kutokana na hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika taarifa, Maher Obeid, mwanachama wa Idara ya Kisiasa ya Hamas, amesema kampeni ya utawala wa Israel ya bomoa bomoa katika wilaya ya Silwan mjini Quds ni sehemu  ya utawala huo ya kuuyahudisha mji huo mtakatifu sambamba na kupora ardhi zaidi za Palestina.

Afisa huyo wa Hamas amesema sera ya Israel ya kuendelea kubomoa nyumba na majengo ya Wapalestina katika mji wa Quds imepelekea kuwe na udharura wa kuanzisha kampeni ya kitaifa ya kuushinikiza utawala wa Kizayuni usitishe kampeni yake dhidi ya wenyeji wa mji huo.

Wilaya ya Silwan iko nje kidogo ya mji wa kale wa wa Al Quds na aghalabu ya wakaazi wake ni Wapalestina. Uongozi wa Kizayuni katika wilaya hiyo umewataka Wapalestina wabomboe nyumba zaidi kwa kisingizio kuwa ujenzi ulifanyika bila vibali.

Hivi karibuni, Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina ilitahadharisha kuwa, uamuzi mpya wa utawala wa Kizayuni wa kuendelea na hatua zake za kivamizi dhidi ya Quds Tukufu na wakaazi wa mji huo unatekelezwa kwa lengo la kubadilisha ukweli kuhusu mji huo pamoja na historia na utmabulisho wake. Mji wa Quds ni muhimu kwa Waislamu kutokana na kuwepo mjini humo eneo tatu takatifu zaidi la Kiislamu yaani Msikiti wa Al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza kwa Waislamu. Mji huo pia una umuhimu kwa wafuasi halisi wa dini za Kikristo na Kiyahudi.

Utawala wa Kizayuni wa Israel, ambao unapata himaya kamili ya Marekani, umekiuka azimio 2334 la Baraza la Usalama, ambalo Disemba 2016 lilitaka usitishwaji wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. 

Karibu jamii nzima ya kimataifa inasisitiza kuwa hatua ya Israel kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi ni kinyume cha sheria.

3472206

Kishikizo: hamas ، palestina ، quds tukufu ، israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: