IQNA

'Lugha ya Qur'ani' kufunzwa katika Chuo Kikuu cha Sydney Australia

15:49 - January 25, 2021
Habari ID: 3473588
TEHRAN (IQNA) - Somo kuhusu 'Lugha ya Qur'ani Tukufu' litaanza kufunzwa kwa mara ya kwanza kwa wanafunzi wa kugha ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Sydney.

Dkt. Ali Yunis Aldahesh mhadhiri katika Kitivo cha Fasihi katika chuo hicho amesema ameandaa somo hilo jipya kwa lengo la kufunza misingi ya tafsiri ya Qur'ani.

Amesema hii itakuwa mara ya kwanza kwa chuo kikuu Australia kufunza 'Lugha ya Qur'ani'.  Dkt. Ali Yunis Aldahesh amefafanua kuwa kuna tafauti baina ya Kiarabu kilichotumika katika Qur'ani na Kiarabu kinachotumika katika vyombo vya habari au vitabu vingine vya masomo na kwa msingi huyo somo hilo limepewa jina la 'Lugha ya Qur'ani.'.

Dkt. Aldahesh amesema atajitahidi kufunza nahw ya Qur'an kwa wanafunzi wa lugha ya Kiarabu. Aidha amesisitiza kuwa somo hilo halitakuwa la kidini au kitheolojia bali litajikita katika kufasiri lugha ya Qur'ani Tukufu.

3949219

Kishikizo: qurani kiarabu australia
captcha