IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
22:06 - August 07, 2020
Habari ID: 3473043
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa mauaji ya watu laki moja katika shambulizi la bomu la nyuklia la Marekani huko Hiroshima ni kielelezo cha tabia na hulka ya kibeberu ya jeshi la nchi hiyo na utovu wa maadili na dini wa Marekani.

Katika ujumbe wake uliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwa mnasaba wa shambulizi la bomu la nyuklia lililofanywa na Marekani huko Hiroshima, Ayatullah Ali Khamenei amesema: Mwezi Agosti mwaka 1945 Marekani ilishambulia mji wa Hiroshima kwa bomu la nyuklia na kuua watu laki moja; hii ndio hulka ya kibeberu ya jeshi la Marekani, kutokuwa na dini, kutomwamini Mwenyezi Mungu na utovu wa maadili Marekani.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kislamu amesisitiza kuwa, iwapo mtu anataka kuzungumzia jinai na uhalifu wa majeshi ya madola ya kibeberu, basi anaweza kuandika vitabu kadhaa.

Tarehe 6 Agosti 1945, ndege ya kivita ya jeshi la Marekani aina ya B-29 ilidondosha bomu la atomiki katika mji wa Hiroshima nchini Japan kwa amri ya rais wa wakati huo wa Marekani, Harry Truman.

Siku tatu baadaye, Marekani iliwadondoshea bomu jengine la atomiki raia wa Japan wa mji wa Nagasaki. Watu wapatao 220,000 walipoteza maisha kutokana na mashambulio hayo mawili yaliyofanywa na Marekani na maelfu ya wengine walijeruhiwa. 

Itakumbukwa kuwa Marekani ndiyo nchi pekee duniani iliyowahi kutumia mabomu ya nyuklia dhidi ya binadamu na hadi sasa haijawahi kuomba radhi kutokana na mauaji hayo ya kinyama.  

Naye

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa kauli kwa mnasaba wa siku ambayo Marekani ilidondosha mabomu ya atomiki huko Hiroshima Japan wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na kusema jinamizi la silaha za atomiki linapaswa kufika ukingoni.

Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran siku ya Alhamisi aliandika ujumbe kwa mnasaba wa mwaka wa 75 wa shambulizi la atomiki la Marekani dhidi ya mji wa Hiroshima nchini Japan katika siku za mwisho za Vita vya Pili vya Dunia na kusema: Miaka 75 iliyopita katika siku kama hii, Marekani ilipata sifa mbaya ya kuwa nchi ya kwanza na ya pekee ambayo imewahi kutumia silaha za atomiki ambazo ziliwalenga watu wasio na hatia."

Zarif amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ni kati ya wamiliki wakubwa zaidi wa silaha za atomiki katika eneo la Asia Magharibi na kuongeza kuwa: "Leo silaha za atomiki za Marekani na Israel ni tishio kwa eneo." 

2786521

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: