IQNA

1,700 wajisajili kushiriki mashindano ya kitaifa Qur’ani Oman

17:41 - August 08, 2020
Habari ID: 3473046
TEHRAN (IQNA) – Watu 1,700 wamejisajili kushiriki katika Mashindano ya 30 ya Qur’ani Tukufu nchini Oman.

Afisa mwandamizi wa mashindano hayo Ali bin Abdullah al-Saqri amesema zoezi la kuwasajili washiriki wa mashindano hayo, ambayo yamepewa jina la mafalme wa zamani wa nchi hiyo, Sultan Qaboos bin Said Aal Said, lilimalizika Jumatano.

Amesema mashindano hayo yana kategoria saba za kuhifadhi na kusoma Qur’ani na kwamba yatafanyika katika miji na mikoa mbali mbali nchini humo.

Afisa mwandamizi wa mashindano hayo Ali bin Abdullah al-Saqri amesema zoezi la kuwasajili washiriki wa mashindano hayo, ambayo yamepewa jina la mafalme wa zamani wa nchi hiyo, Sultan Qaboos bin Said Aal Said, lilimalizika Jumatano.

Amesema mashindano hayo yana kategoria saba za kuhifadhi na kusoma Qur’ani kwa mbinu ya tartil. Katika kuhifadhi Qur’ani kutakuwa na kategoria mbili za kuhifadhi Qur’ani kikamilifu na kuhifadhi juzuu mbili.

Awali mashindano hayo yatafanyika katika ngazi ya mikoa na miji ili kuwachagua watakaofika finali.

3915239

captcha