IQNA

Hizbullah yatoa wito wa kufanyika maombolezo ya Muharram majumbani

18:07 - August 11, 2020
Habari ID: 3473057
TEHRAN (IQNA) – Harakati za Hizbullah na Amal nchini Lebanon zimetoa wito kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo kufanya maombolezo ya Imam Hussein AS katika Mwezi wa Muharram mwaka huu majumbani.

Katika taarifa ya pamoja, harakati hizo mbili za mapambano ya Kiislamu zimetoa wito kwa waumini kufuata maagizo ya viongozo wa kidini kuhusu kutoandaa mijimuiko na misafara mikubwa katika mwezi wa Muharram kutokana na janga la corona au COVID-19. Taarifa ya Hizbullah na Amal imesema wanaomuomboleza Imam Hussein AS wanapaswa kuzingatia maagizo yote ya kiafya wakati wa maombolezo.

Halikadhalika harakati hizo mbilo zimeshauri kufanya hafla ndogo za maombolezo majumbani, kutoa hotuba kupitia mitandao ya kijamii na intaneti, kusambaza ujumbe wa Ashura kupitia upandishaji bendera nyeusi na kuandika mabango yenye jumbe za mnasaba huu.

Katika mwezi wa Muharram Waislamu, hasa Waislamu wa madhehebu ya Shia hujumuika kuomboleza kuuawa shahidi kikatili mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS mwaka wa 61 Hijria katika jangwa la Karbala nchini Iraq akiwa. Imam Hussen AS na wafuasi wake watiifu 72, waliuawa shahidi tarehe 10 Muharram, ambayo ni maarufu kama Siku ya Ashura.

Kufuatia kuibuka janga la corona,mijumuiko mingi ya kidini, kijamii, kisiasa, kimichezo n.k imepigwa marufuku kote duniani ili kuzuia kuenea ugonjwa huo hatari.

3915871

 

captcha