IQNA

Kituo kikubwa cha kufunza Qur’ani chfunguliwa Nigeria

19:00 - September 03, 2020
Habari ID: 3473133
TEHRAN (IQNA) –Kituo Jumuishi cha Kufunza Qur’ani (IQE) kimefunguliwa katika jimbo la Niger nchini Nigeria.

Akifungua kituo hicho, gavana wa jimbo la Niger amesema kituo hicho kitawawezesah wanafunzi kuhifadhi Qur’ani Tukufu na wakati huo huo kuendelea na masomo ya kawaida ya mfumo wa kitaifa wa shule za msingi.

Amesema uzinduzi wa shule hiyo utawawezesha wanafunzi kuweza kupata ujuzi katika taaluma zingine maishani sambamba na kuhifadhi Qur’ani na hivyo kuzuia tatizo la watoto wengi wanaosoma madrassa kuishia kuombaomba mitaani. Watoto hao ambao kama ni maarufu kama Almajiri wamekuwa kero kubwa katika majimbo ya kaskazini mwa Nigeria.

Gavana huyo ametoa wito kwa wazazi kutumia vizuri chuo hicho kuwasajili watoto wao katika shule hiyo yenye masomo ya Qur’ani na masomo ya kisekula. Kuna mpango wa kujenga shule kama hizo katika maeneo mbali mbali ya kaskazini mwa Nigeria.

3920513

captcha