IQNA

Waislamu Nigeria

Kozi za Kuhifadhi Qur'ani zazinduliwa katika Mji Mkuu wa Nigeria

15:42 - September 23, 2024
Habari ID: 3479475
IQNA - Shule ya Amirul Muminin (AS) huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria, imezindua kozi za kuhifadhi Qur'ani kwa wavulana na wasichana.

Kozi hizo zilianza wiki iliyopita na zitadumu kwa miezi miwili. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO), shule hiyo inafungamana na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Nigeria.

Masomo hayo yanafundishwa na walimu wa Qur'ani Wanigerai, kulingana na ripoti hiyo.

Majid Kamrani, Mwambata wa Utamaduni wa Iran, alisema katika sherehe za ufunguzi kwamba kozi hizo hufanyika Jumamosi na Jumapili katika vikundi viwili tofauti vya wavulana na wasichana.

Amesisitiza kuwa kufahamiana na Qur'ani Tukufu na kufanya juhudi za kufaidika na mafundisho yake sio tu kuna baraka za kimaanawi kwa watu binafsi, familia na jamii bali pia kunaleta amani na ustawi maishani.

Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Nigeria kimeweka ajenda yake ya kutumia uwezo wa taasisi za kidini na mashinani kuendeleza shughuli za Qur'ani.

Nigeria ni nchi iliyoko kwenye Ghuba ya Guinea huko Afrika Magharibi.

Takriban asilimia 50 ya wakazi wa nchi hiyo wanakadiriwa kuwa Waislamu, wakati asilimia 40 ni Wakristo na 10 wanafuata dini za kienyeji.

3489991

Habari zinazohusiana
captcha