IQNA

Nchi 20 kushiriki mashindano ya Qur’ani ya kimataifa nchini Nigeria

19:20 - May 03, 2025
Habari ID: 3480632
IQNA – Nigeria inapanga kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu na kushirikisha maqari wa Qur’ani kutoka nchi 20.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Muhammad Bashir kwa niaba ya kamati ya uandaaji ya mashindano hayo, tukio hili linatayarishwa na taasisi ya 'Majalisu Ahlil Quran International Quranic Competition'.

Mashindano hayo yatawaleta pamoja washiriki kutoka kote duniani. Mashindano haya, yanayoongozwa na aliyekuwa mbunge wa shirikisho Mheshimiwa Muhammad Adam Alkali, ambaye aliwakilisha Bassa/Jos North katika Jimbo la Plateau, yanatarajiwa kufanyika Agosti 2025.

 Tukio hili litaanza huko Jos, Jimbo la Plateau, na kilele chake kitafanyika katika jiji kuu la Abuja. "Katika mkutano wa maandalizi uliofanyika hivi karibuni, Mheshimiwa Alkali alieleza shukrani kubwa kwa msaada imara kutoka kwa Kituo cha Masomo ya Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Usman Danfodio, Sokoto.

"Amesisitiza lengo la mashindano haya kukuza maadili ya Kiislamu na umoja, huku akibainisha kuwa Qur’ani Tukufu  ni kama mwanga unaoongoza Waislamu katika kutafuta maisha yenye maana," ilisema taarifa hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya uandaaji, Gwani Sadiq Zamfara, pia alitoa taarifa kuhusu maandalizi, akihakikishia kwamba mipango yote iko sawa ili kuhakikisha tukio linakwenda vizuri na kwa mafanikio.

Nchi zinazotarajiwa kushiriki ni pamoja na Nigeria, Cameroon, Ghana, Chad, Senegal, Kenya, Tanzania, Mauritania, Niger, Misri, Morocco, Libya, Algeria, Saudi Arabia, Kuwait, Qatar, Malaysia, Uingereza, Umoja wa Falme za Kiarabu, na Marekani.

3492908

Habari zinazohusiana
captcha