IQNA

Waserbia tisa waliohusika na mauaji ya 1992 ya Waislamu Bosnia wakamatwa

18:19 - September 17, 2020
Habari ID: 3473179
TEHRAN (IQNA) – Polisi nchini Bosnia wamewakamata Waserbia tisa ambao wanashukiwa kuhusika na mauaji ya Waislamu 44 katika kijiji kimoja mwanzoni mwa vita vya Bosnia mwaka 1990.

Wanaume hao tisa ni wanajeshi waliostaafu na makamanda wawili wa polisi waliostaafu na wanashukiwa kupanga na kushiriki katika mauaji na ukandamizaji wa Waislamu katika eneo la Sokolac mashariki mwa Bosnia mnamo Septemba 1992.

Itakumbukwa kuwa, miaka 25 iliyopita katika siku kama ya jana, Waislamu zaidi ya elfu nane wa mji wa Srebrenica mashariki mwa Bosnia Herzegovina waliuawa kwa umati.

Mauaji hayo yalifanywa na Waserbia wenye misimamo mikali. Maafa hayo yalikuwa mauaji makubwa zaidi ya halaiki kuwahi kutokea barani Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Wakati wa mauaji hayo ya kimbari, wanajeshi wa kulinda amani wa Uholanzi waliokuweko katika eneo hilo hawakuchukua hatua yoyote ya kuwahami Waislamu hao wa Srebrenica. 

 Jenerali Ratko Mladic, aliyekuwa kamanda wa kijeshi wa Serbia na ambaye aliongoza mauaji hayo ya Waislamu 8,000 wa Bosnia alihukumiwa maisha jela Novemba 2017, miaka 20 baada ya mauaji hayo ya kimbari.

3472590

Kishikizo: bosnia herzegovina ، waislamu ، serb
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :