IQNA

22:36 - July 12, 2021
News ID: 3474094
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema mauaji ya Waislamu wa katika mji wa Srebrenica ni ukurasa mchafu katika historia ya mwanadamu wa leo.

Katika ujumbe wake uliosomwa Jumapili kwa mnasaba wa mwaka wa 26 wa mauaji ya Srebrenica, amesema mauaji hayo ni jeraha la kina katika dhamira ya mwanadamu.

Ujumbe huo ulisomwa na mjumbe maalumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ebrahim Taherian. Zarif ameongeza kuwa wanawake na kinamama wa Srebrenica bado wanataka uadilifu  utendeke.

Ameendelea kusema kuwa maadhimisho ya Jumapili ya mauaji hayo ni ujumbusho kwa jamii ya kimataifa kuhusu haja ya uadilifu kutendeka.

Aidha amemsema Iran ina fahari kuwa ilisimama bega kwa began a watu wa Bosnia Herzegovina tukoa walipopata uhuru na haiwezi kustia kuendelea kulisaidia taifa hilo.

Ikumbukwe kuwa, 11 Julai mwaka 1995, Waislamu zaidi ya elfu nane wa mji wa Srebrenica mashariki mwa Bosnia Herzegovina waliuawa kwa umati.

 Mauaji hayo yalifanywa na Waserbia wenye misimamo mikali. Maafa hayo yalikuwa mauaji makubwa zaidi ya halaiki kuwahi kutokea barani Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Wanamgambo wa Kiserbia wakiungwa mkono na serikali ya Belgrade, waliuvamia mji wa Srebrenica licha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulitangaza eneo hilo kuwa la amani mwaka 1993 na kutumwa askari wa umoja huo katika mji huo.

Waislamu wa mji wa Srebrenica walijaribu kuondoka katika mji huo, lakini watenda jinai wa Kiserbia waliwauwa wanaume na watoto wao wa kiume na kuwaruhusu wanawake kuondoka katika mji huo. Wakati wa mauaji hayo ya kimbari, wanajeshi wa kulinda amani wa Uholanzi waliokuweko katika eneo hilo hawakuchukua hatua yoyote ya kuwahami Waislamu hao wa Srebrenica.  

3983414

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: