IQNA

Ujerumani yampokonya tuzo Mzayuni aliyekana mauaji ya Waislamu wa Bosnia

12:28 - January 01, 2022
Habari ID: 3474750
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Ujerumani imebatilisha uamuzi wake wa kumuenzi mwanahistoria wa utawala wa Kizayuni wa Israel baada ya matamshi yake ya kukana mauaji ya Waislamu.

"Pendekezo la Kump Profesa Gideon Greif Tuzo ya Order of Merit ya Ujerumani limefutwa," imetangaza Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani Alhamisi.

Ujerumani imekosolewa vikali kufuatia uamuzi wake wa kumtunuku Greif Tuzo hiyo kutokana na utafiti wake kuhusu kambi ya Auschtwitz.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani imeashiria kazi ya Tume ya Ujerumani ya Srebrenica, eneo ambalo Waislamu 8,000 wa Bosni Hezorgovina waliuawa. Waizara ya Mambo ya Nje ya Ujeurmani imesema matokeo ya uchunguzi wa tume hiyo yamekiuka maamuzi ya Makamam ya Kimataifa ya Jinai za Yugoslavia ya Zamani, Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu na Mkatba wa Kimataifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari.

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema kufutwa tuzo hiyo kumetokana na hatua ya Greif akiwa kama mwenyekiti wa tume hiyo hiyo kudunusha mauaji ya Waislamu wa Bosnia ambao waliangamizwa kwa umatu na Waserbia mwaka  1995 katika eneo la Srebrenica.

Tume hiyo ilidai kuwa mauaji ya Waislamu wa Srebrenica hayakuwa mauaji ya kimbari.

Ikumbukwe kuwa, 11 Julai mwaka 1995, Waislamu zaidi ya elfu nane wa mji wa Srebrenica mashariki mwa Bosnia Herzegovina waliuawa kwa umati.

 Mauaji hayo yalifanywa na Waserbia wenye misimamo mikali. Maafa hayo yalikuwa mauaji makubwa zaidi ya halaiki kuwahi kutokea barani Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Wanamgambo wa Kiserbia wakiungwa mkono na serikali ya Belgrade, waliuvamia mji wa Srebrenica licha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulitangaza eneo hilo kuwa la amani mwaka 1993 na kutumwa askari wa umoja huo katika mji huo.

Waislamu wa mji wa Srebrenica walijaribu kuondoka katika mji huo, lakini watenda jinai wa Kiserbia waliwauwa wanaume na watoto wao wa kiume na kuwaruhusu wanawake kuondoka katika mji huo. Wakati wa mauaji hayo ya kimbari, wanajeshi wa kulinda amani wa Uholanzi waliokuweko katika eneo hilo hawakuchukua hatua yoyote ya kuwahami Waislamu hao wa Srebrenica.  

3477170

captcha