IQNA

Waislamu wa Bosnia wakumbuka mauaji ya Srebrenica

19:46 - July 11, 2021
Habari ID: 3474091
TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya Waislamu wa Bosnia Herzegovina wamekusanyika leo Jumapili kuwakumbukwa wenzao waliouawa uaawa vitani miaka 26 iliyopita

Siku kama hii ya 11 Julai mwaka 1995, Waislamu zaidi ya elfu nane wa mji wa Srebrenica mashariki mwa Bosnia Herzegovina waliuawa kwa umati.

 Mauaji hayo yalifanywa na Waserbia wenye misimamo mikali. Maafa hayo yalikuwa mauaji makubwa zaidi ya halaiki kuwahi kutokea barani Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Wanamgambo wa Kiserbia wakiungwa mkono na serikali ya Belgrade, waliuvamia mji wa Srebrenica licha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulitangaza eneo hilo kuwa la amani mwaka 1993 na kutumwa askari wa umoja huo katika mji huo.

Waislamu wa mji wa Srebrenica walijaribu kuondoka katika mji huo, lakini watenda jinai wa Kiserbia waliwauwa wanaume na watoto wao wa kiume na kuwaruhusu wanawake kuondoka katika mji huo. Wakati wa mauaji hayo ya kimbari, wanajeshi wa kulinda amani wa Uholanzi waliokuweko katika eneo hilo hawakuchukua hatua yoyote ya kuwahami Waislamu hao wa Srebrenica.  

Mwezi uliopita wa Juni, majaji wa Mahakama ya Jinai za Kivita ya Umoja wa Mataifa wamedumisha hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya Jenerali Ratko Mladic, aliyekuwa kamanda wa kijeshi wa Serbia, ambaye mwaka 2017 alipatikana na hatia ya kuagiza na kuongoza mauaji ya maelfu ya Waislamu huko Srebrenica. 

3475204

captcha