IQNA

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kuhusu madai ya Marekani kurejesha vikwazo

20:14 - September 20, 2020
Habari ID: 3473186
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumapili imetoa tamko rasmi na kusema kuwa, Marekani ndiye mhatarishaji mkubwa wa usalama na amani katika kona zote za dunia.

Katika taarifa yake hiyo rasmi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema, leo Marekani imezusha uongo mwingine wa kudai kurejea maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu vikwazo vya Baraza la Usalama dhidi ya Iran na kusema kuwa, pamoja na kwamba madai hayo ya uongo ya Marekani yamekataliwa na kila upande kutokana na kwamba Washington si mwanachama tena wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, lakini pia mchakato huo hata kuanza haujaanza vipi leo Marekani itadai umeshafikia mwisho?

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, hata waziri wa mambo ya nje wa Marekani mwenyewe anatambua kwamba madai yake ya kurejea vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran ni ya uongo na hayana msingi wowote na ndio maana ameamua kutoa vitisho kwa nchi nyingine kuwa Marekani itaziwekea vikwazo, vitisho ambavyo vyenyewe ni ushahidi wa wazi kabisa wa kukiri Washington kuwa imefeli.

Sehemu nyingine ya tamko rasmi la Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema, Tehran inayahesabu madai yaliyojaa chuki ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani dhidi yake kuwa yanatolewa kwa ajili ya matumizi ya kisiasa ya ndani ya Marekani tu na yanatokana na mtu aliyeshindwa, aliyekata tamaa, aliyeemewa na asiyejua la kufanya. 

Ikumbukwe kuwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, Marekani imekuwa ikila mweleka mtawalia mbele ya Iran. Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema katika taarifa yake hiyo ya leo kuwa inampa nasaha (za bure) rais wa Marekani kwamba aache kufuata ushauri wa watu majahili na wajinga ambao hawana welewa na masuala ya dunia ili aweze kuikoa nchi yake isizidi kutengwa kimataifa.

3924099/

Kishikizo: iran ، marekani ، vikwazo
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :