IQNA

Msikiti wenye mvuto huko Malang, Indonesia + Video na Picha

11:20 - November 11, 2020
Habari ID: 3473349
TEHRAN (IQNA) – Masjid Tiban msikiti maridadi na wenye mvuto katika mji wa Malang nchini Indonesia.

Mji wa Malang uko katika mkoa wa Java Mashariki nchini Indonesia.

Masjid Tiban umejengwa katika kiwanja chenye ukubwa wa hekari sita.

Ujenzi wa msikiti huo ulianza mwaka 1968 na kukamilika 1978.

Maelfu ya watalii kutoka Indonesia na nchi jirani kama vile Brunei na Malaysia huutembelea msikiti huo kila siku.

Mbali na kutumika kama eneo la ibada, msikiti huo pia una chuo cha kiislamu cha bweni na halikadhalika maktaba ya vitabu vya Kiislamu, mgahawa na akuariamu.

Usanifu majengo wa msikiti huo umetegemea mitindo ya usanifu majengo wa Kiarbau, Kithai na Java Mashariki.

3473089

 
 
 
captcha