Njia ya udugu yenye urefu wa mita 28.3, inayojulikana kama Terowongan Silahturahmi, inaunganisha Msikiti wa Istiqlal - msikiti mkubwa zaidi wa Asia ya Kusini-Mashariki - na Kanisa la Assumption Cathedral.
Her Pramtama, mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Msikiti wa Istiqlal, alisema kuwa timu kwa sasa inaunda mchoro wa njia hiyo ya chini ya ardhi.
Katika njia hiyo wageni watakumbana na nukuu kutoka kwa Uislamu na Ukatoliki kuhusu umuhimu wa udugu kwenye lango la njia hiyo. Rais Joko Widodo anatazamiwa kuzindua njia hiyo ya chini ya ardhi mwezi Agosti, ingawa tarehe kamili haijathibitishwa.
Padre Anthonius Gregorius Lalu, naibu mratibu wa mahusiano ya vyombo vya habari wa kamati ya ziara ya Papa, alitaja kuwa Papa atatembelea kanisha hilo mnamo Septemba 4 . Siku inayofuata, atatembelea Msikiti wa Istiqlal kwa ajili ya mkutano wa wafuasi wa dini mbalimbali.
3489258