IQNA

Maelfu ya Wapalestina washiriki swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Aqsa

21:08 - November 14, 2020
Habari ID: 3473360
TEHRAN (IQNA)- Malefu ya Wapalestina wameshiriki katika Swala ya Ijumaa wiki hii katika Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel.

Kwa mujibu wa taarifa idadi kubwa ya Wapalestina waliingia katika msikiti huo pamoja na kuwepo vizingiti ambavyo vimewekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika hotuba yake ya Swala ya Ijumaa, Imamu wa Msitiki wa Al Aqsa alilaani vikali hatua ya Ufaransa kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW. Aidha ametoa wito kwa Waislamu kususia bidhaa za Ufaransa kama njia ya kubainisha malalamiko yao.

Utawala wa Kizayuni huwazuia Wapalestina wengi kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa kwa ajili ya Swala ya Ijumaa huku walowezi wa Kizayuni wakiruhusiwa kuingia katika eneo hilo takatifu la Waislamu bila vizingiti.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

3934958

captcha