IQNA

Malefu washiriki Swala ya Ijumaa katika qibla cha kwanza cha Waislamu

19:07 - December 18, 2020
Habari ID: 3473467
TEHRAN (IQNA) – Maelfu ya Wapalestina leo wamshiriki katika Swala ya Ijumaa katika kibla cha kwanza cha Waislamu, yaani Msikiti wa Al Aqsa ulioko mjini Quds (Jerusalem).

Kwa mujibu wa taarifa, Wapalestina wanaoishi walianza kufika katika Msikiti wa Al Aqsa mapema Ijumaa asubuhi ambapo wameshiriki katika Swala ya Ijumaa kwa kuzingatia kanuni za kiafya za kuzuia kuenea corona.

Imearifiwa kuwa wanajeshi wa utawala haramu wa Israel ambao unakalia Quds kwa mabavu, waliweka vituo vya upekuzi katika milango ya kuingia Msikiti wa Al Aqsa ambapo walichunguza vitambulisho vya Wapalestina na kuwazuia wengine kuingia eneo hilo takatifu.

Khatibu wa  Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Aqsa Sheikkh Yusuf Abu Sunaina  aliwashukuru Wapalestina wanaoishi Quds kwa kujitokeza wka wingi katika Swala ya Ijumaa na kusema nukta hiyo inaashiria wanafungamana kikamilifu na kuuhami Msikiti wa Al Aqsa.

Sheikh Abu Sunaina amekumbusha kuwa Waislamu ndio wamiliki wa Msikiti wa Al Aqsa na hata pamoja na kuwepo jinai na hujuma za Wazayuni dhidi ya msikiti huo, wataendelea kuulina.

Aidha ametoa wito kwa Wapalestina kujitokeza nyakati zote katika Msikiti wa  Al Aqsa ili kuulinda.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel, ambapo unakalia Palestina kwa mabavu, umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina. Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

3941818

captcha