IQNA

Hamas yalaani UAE kwa kuunga mkono Israel katika ujenzi wa vitongoji haramu

19:44 - November 16, 2020
Habari ID: 3473364
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali utawala wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kutokana na uungaji mkono wake kwa ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Katika taarifa Jumapili, msemaji wa Hamas Hazem Qassem amesema UAE hivi karibuni ilimpokea  mkuu wa  ‘Baraza la Vitongozji vya Wazayuni’ katika Ukingo wa Magharibi ambapo pande mbili zilitiliana saini mapatano ya ushirikiano wa kiuchumi.

Hamas imesema safari ya UAE ya Yossi Dagan, mkuu wa Baraza la Israel la Vitongoji katika Ukingo wa Magharibi na utiwaji siani mapano ya ushirikiano wa kibiashara baina ya pande mbili ni ‘uungaji mkono wa kivitendo’  wa UAE kwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina.

Hayo yanajiri wakati ambao Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya ametoa taarifa akipinga vikali ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zilizobandikwa jina la Israel. Josep Borrell sambamba na kueleza msimamo wa Umoja wa Ulaya wa kupinga ujenzi wa vitongoji hivyo vipya vya walowezi wa Kizayuni ameonyesha wasiwasi mkubwa aliona kwa hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sahemu moja ya taarifa yake imesema: Nina wasiwasi mkubwa na uamuzi wa Israel wa kuanza kujenga nyumba mpya 1,257 katika fremu ya mpango wa ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika kitongoji cha Givat Hamatos.

Hadi sasa hakujachukuliwa hatua yoyote ya kutekeleza azimio nambari 2234 la tarehe 23 Disemba 2016 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel. 

3473130

captcha