IQNA

Qiraa yenye mvuto ya Ustadh Abdul-Basit

17:12 - November 27, 2020
Habari ID: 3473400
TEHRAN (IQNA)- Klipu ya Ustadh Abdul-Basit Abdul-Swamad akisoma aya za Sura Ash-Shu’araa katika Qur’ani Tukufu imeseambazwa katika mitandao ya kijamii.

Katika klipu hii Ustadh Abdul-Basit anasema aya za 78-81 za Sura Ash-Shu’araa.

Sheikh Abdul Basit Abdul Samad alizaliwa mwaka 1927 katika kijiji cha Almazaizah katika eneo la Armant kusini mwa Misri. Sheikh Abdul Basit Abdul Swamad alikamilisha hifdhi ya Qur'ani akiwa na umri wa miaka 10 kijijini kwake kwa Ustadh Al Amir na akahitimu aina zote za kiraa ya Qur'ani akiwa na umri wa miaka 14.

Abdul Basit alipewa lakabu ya 'Koo ya Dhahabu' kutokana na kiraa yake ya kuvutia na alipendwa mno na wafuatiliaji wa masuala ya Qur'ani kwa kadiri kwamba hadi sasa anatambuliwa kuwa qarii mashuhuri na anayepesndwa zaidi wa Qur'ani.

Qari huyo mashuhuri wa Misri aliaga dunia tarehe 30 Novemba mwaka 1988 katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

937604

captcha