IQNA

Msikiti wa Kutubiyya, nchini Morocco, adhama ya usanifu majengo wa Kiislamu

21:47 - December 05, 2020
Habari ID: 3473424
Msikiti wa Kutubiyaa, ni msikiti mkubwa zaidi katika mji wa Marakesh, nchini Morocco na pia ni moja kati ya misikiti muhimu zaidi nchini humo.

Msikiti huo uko katika mtaa wa Jemaa el-Fna mjini Marakesh ambao hutembelewa sana na watalii.

Msikiti wa Kutubiyaa uliasisiwa mwaka 1147 Miladia na khalifa Abd al-Mu’min alyekuwa akitawala katika zama za silsila ya watawala wa Almoahad na kisha ukkakarabatiwa upya mwaka 1158. Msikiti huo umejengwa kwa usanifu majengo wenye mvuto wa Kiislamu. Minbar ya msikiti huu, ambayo ni kielelezo cha ustadi wa sanaa ya Kiislamu, ilijengwa katika karne ya 12 Miladia katika mji wa Cordoba nchini Uhispania.

 
 
captcha