IQNA

Iran yachapisha nakala millioni 2.2 za Qur’ani Tukufu katika kipindi cha miezi 9

20:30 - December 16, 2020
Habari ID: 3473461
TEHRAN (IQNA) – Nakala milioni 2.2. za Qur’ani Tukufu zimechapishwa nchini Iran katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.

Kwa mujibu wa Meysam Moafi, mkurugenzi wa usimamizi wa uchapishaji Qur’ani katika Taasisi ya Darul Qur’an al Karim ya Iran amesema kumekuwa na ongezeko la asilimia 30 la uchapishaji Qur’ani  nchini Qur’ani mwaka huu ikilinagnishwa na wakati sawa na huu mwaka jana.

Ameongeza kuwa,  misahafu inayochapishwa imeongezeka kutokana na kuwa janga la COVID-19 au corona ambalo limepelekea idadi kubwa ya watu walazimika kukaa mmajumbani na wengi wametumia muda huo kusoma Qur’ani Tukufu.

Hali kadhalika amesema kumeshuhudiwa pia ongezeko la utumizi wa nakala za Qur’ani za kidijitali  katika intaneti na aplikesheni za simu za mkononi.

3941207

captcha