Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Darul Qur'an Karim la Iran kumekuwa na ongezeko la asilimia 20 la uchapishaji Misahafu au Nakala za Qur'ani Tukufu ikilinganishwa na wakati mshabaha mwaka jana.
Katika mahojiano na IQNA, amesema vibali 88 vimepewa mashirika mbali mbali kuchapisha misahafu mwaka huu.
Shirika la Darul Qur'an Karim linafungamana na Shirika la Ustawi wa Kiislamu Iran na huwa na jukumu la kusimamisha uchapishaji nakala za Qur'ani nchini Iran.