IQNA

Harakati za Qur'ani

Kituo cha Dar-ul-Quran Karbala kuandaa kozi za Qur'ani Mtandaoni kwa wahitimu

23:26 - July 26, 2024
Habari ID: 3479187
IQNA - Kituo cha Da-ul-Quran cha Idara ya Mfawidhi wa Kaburi Takatifu la Imam Hussein (AS) huko Karbala, Iraq kinapanga kuandaa kozi za mtandaoni za Qur'ani kwa wahitimu wa vyuo vikuu katika fani tofauti za sayansi ya Qur'ani

Karrar al-Shamari, ambaye ni msimamizi wa ofisi ya habari ya kituo hicho, alisema kozi hizo za juu zitatolewa katika nyanja tofauti za Qur'ani.

Alisema mafunzo hayo yanalenga kuinua kiwango cha elimu ya Qur'ani kwa wahitimu hao.

Baada ya kufaulu kila kozi kwa mafanikio, wanaweza kuchukua kozi ya kiwango cha juu, alibainisha.

Al-Shamari pia alisema kituo hicho kinaandaa kozi  za kiwango cha msingi za Qur'ani za usomaji katika mji mtakatifu wa Najaf na katika mji wa kusini wa Basra.

Madhumuni ya kozi hizo ni kukuza mafundisho ya Quran na Ahl-ul-Bayt (AS) na kuimarisha uhusiano wa familia na Qur’ani Tukufu, aliendelea kusema.

Shughuli za Qur'ani zimeendelea kwa kiasi kikubwa nchini Iraq tangu kupinduliwa kwa dikteta wa zamani Saddam Hussein mwaka 2003.

Kumekuwa na mwelekeo unaokua wa programu za Qur'ani kama vile mashindano, vipindi vya kisomo na programu za elimu zilizofanyika nchini katika miaka ya hivi karibuni.

3489243

Habari zinazohusiana
Kishikizo: darul quran karbala
captcha