Hayo yamedokezwa na Sayyid Hossein Mousavi Baladeh, mkuu wa masuala ya Qur’ani katika Baraza la Jiji la Tehran katika mahojiano na IQNA.
Ameongeza kuwa, kufuatia kulegezwa sheria za kuzuia kuenea COVID-19 baada ya maambukizi kupungua, hvi sasa Vituo vya Masomo ya Qur’ani sasa vitaanza masomo kwa kuhudhuria wanafunzi na waalumu ana kwa ana.
Amesema hivi sasa kuna taasisi 11 za Darul Qur’an ambazo zinafungamana na Baraza la Jiji la Tehran ambapo mbali na kutoa mafunzo kwa umma pia hutumika kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa baraza hilo.
Aidha ameelezea matumaini kuwa bajeti ya vituo vya Qur’ani itaongezwa ili kustawisha zaidi harakati za Qur’ani katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.