IQNA

Algeria yaafiki kufungua tena Madrassah za Qur'ani

18:57 - January 01, 2021
Habari ID: 3473514
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Algeria imeafiki kufunguliwa tena madrassah za Qur'ani Tukufu nchini humo ambazo zilikuwa zimesitisha shughuli zao kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Katika taarifa siku ya Alhamisi, 31 Disemba 2020, Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini Algeria imesema madrassah za Qur'ani nchini humo zitafunugliwa kwa sharti la kuzingatia kikamilifu kanuni maalumu zilizowekwa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Taarifa hiyo imesema, wakuu wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini watashirikiana na serikali za mitaa kusimamia madrassah hizo za Qur'ani na kuhakikisha kuwa zinaendesha shughuli zao kwa mujibu wa taratibu zilizoko.

Aidha wizara hiyo imetahadahrisha kuwa itafunga madrassah yoyote ambayo itakiuka sheria za kukabiliana na corona.

Hivi karibuni Jumuiya ya Maulamaa Algeria ilitaka madrassah za Qur'ani nchini humo zifunguliwe kwa kuzingatia kanuni za kukabiliana na corona.

Hadi kufikia Januari 1 2021, waliambukizwa corona Algeria walikuwa wamefika 99,610 huku waliofariki wakiwa ni 2,756.

3944821

captcha