IQNA

Jeshi la utawala wa Israel labomoa msikiti Ukingo wa Magharibi

20:29 - January 27, 2021
Habari ID: 3473596
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamebomoa msikiti na majengo kadhaa ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Kwa mujibu wa taarifa buldoza za jeshi la utawala dhalimu wa Israel zimebomoa msikiti ambao ulikuwa unajengwa katika mji wa Umm Qusah kusini mwa eneo la Al Khalil. Muhammad Yatimin, mkurugenzi wa shule moja iliyo karibu na msikiti huo amesema wakuu wa utawala dhalimu wa Israel wamedai kuwa eti msikiti huo haukuwa na kibali cha ujenzi.

Buldoza hizo za utawala wa Israel pia zimeharibu shamba la mifugo mashariki mwa Quds (Jerusalem).

Utawala wa kikoloni wa Israel unakalia kwa mabavu ardhi za Palestina na unawanyima Wapalestina haki ya kutumia ardhi zao watakavyo. Wakati huo huo utawala huo dhalimu unaendeleza ujenzi wa vitongozji vya walowezi wa Kizyauni katika ardhi unazozipora za Wapalestina katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi.

Kwa mujibu wa sheria za kimataifa maeneo ya magharibi na mashariki mwa Quds yanatambuliwa kuwa ardhi ambazo zimekaliwa kwa mabavu na hivyo hatua zozote za ujenzi ambazo zinatekelezwa na utawala wa Kizayuni ni kinyume cha sheria.

3473826

captcha