Wanaharakati wa mitandao ya kijamii walianzisha kampeni ya kueleza mshikamano wao na Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili baada ya mhubiri huyo mkuu kutukanwa kwenye X, iliyojulikana kama Twitter, kwa misimamo yake.
Katika chapisho la X, ametangaza mshikamano kamili na watu wa Palestina, wakiwemo Ukanda wa Gaza, pamoja na watu wa Yemen na Lebanon ambao wanakabiliwa na uvamizi wa utawala wa Israel na Marekani.
Vile vile amesifu uwezo wa harakati ya muqawama ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah kwa uwezo wake wa kuilenga Tel Aviv kwa makombora.
Wakati baadhi ya watumiaji wakimkosoa Mufti na kutuma matusi, wengine wengi walimpongeza na kueleza misimamo yake kuwa ni ya ujasiri.
Kwa miaka mingi, Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili amebaki imara katika uungaji mkono wake kwa ajili ya Palestina.
Vile vile amekosoa majaribio ya kuhalalisha uhusiano na utawala wa Israel na kupinga hatua yoyote ya Oman katika mwelekeo huo.
4238462