IQNA

Msemaji wa Harakati ya Nujaba

Ujumbe wa Mapinduzi ya Kiislamu umejikita katika kurejea katika Uislamu halisi

15:28 - February 11, 2021
Habari ID: 3473640
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Nujabaa ya Iraq amesema moja kati ya mafanikio makubwa zaidi ya Mapinduziya Kiislamu ya Iran ni kuwezesha kurejea Uislamu halisi duniani.

Nasr al-Shammari ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na IQNA kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano hayo.

Swali: Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwa na taathira katika nchi zote za Kiislamu ikiwemo Iraq ambayo mbali na kupakana na Iran pia sawa na Iran ina idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Shia. Unaweza kutufahamisha namna ambavyo Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliathiri harakati za Kishia nchini Iraq.?

Jibu: Kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hakukuwa na muelekeo maalumu wa kisiasa miongoni mwa Mashia wa Iraq. Aghalabu ya vijana walikuwa ima wanafuata vyama vya uliberali wa Kimagharibi, Ukomunisti au Ushocialisti. Kabla ya mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hakukuwa na harakati yenye nguvu ya Kishia Iraq isipokuwa harakati ya Shahidi Al-Sadr na Chama cha Kiislamu cha Da'wah ambayo kilihujumiwa na utawala wa kifashisti wa chama cha Baath, utawala ambao ulikuwa unaungwa mkono na kambi za Magharibi.  Hujuma hiyo ilifika kileleni kwa kuuawa shahidi Ayatullah Muhammad Baqir al-Sadr na dada yake ambao walihukumiwa kifungo cha kunyongwa Aprili 9, 1980. Ayatullah al-Sadr alikuwa muungaji mkono mkubwa Mapinduzi ya Kiisalmu yaliyojiri Februari 1979. Msimamo huo wa Ayatullah al-Sadr ulipelekea vijana wengi Iraq waunge mkono Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Swali: Kwa kuzingatia nukta hiyo uliyoitaja unaweza kusema ni vipi Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwa na taathira katika kuwawezesha Wairaqi kukabiliana na makundi ya Mawahhabi Wakufurishaji kama vile al-Qaeda na ISIS.

Jibu: Kabla sijazungumza kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu, nigependa kwanza tuwe na taswira ni yapo yangejiri iwapo hakungekuwa na Jamhuri ya Kiislamu katika eneo. Ni wazi kuwa kungekuwa na tawala za Kiwahhabi katika eneo ambazo zingevuruga usalama kama ambavyo leo tunaona Marekani na Israel zimefurahia na hata zimeunga mkono uwepo wa makundi ya magaidi Mawahabbi wakufirishaji. Kwa hivyo kama Mapinduzi ya Kiislamu hayangekuwepo leo, eneo hilo lote halingeweza kukabiliana na harakati za magaidi wakufurishaji.

Swali: Je, fikra za kisiasa za Imam Khomeini, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu, zimekuwa na taathira gani katika Mhimili wa Muqawama au mapambano ya Kiislamu hasa kwa kuzingatia mhimili huu unakabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel na madola ya kibeberu na kiistikbari?

Jibu: Harakati ya mapambano ya Kiislamu au muqawama ambayo iliibuliwa na Imam Khomeini iliweza kuushinda utawala wa Kizayuni wa Israel na kukomboa ardhi za Lebanon zilizokuwa zinakaliwa kwa mabavu na utawala huo. Harakati ya muqawama imeweza kusambaratisha ile dhana potovu kuwa jeshi la Israel haliwezi kushindwa. Marekani pia ilikuwa na kikosi kikubwa zaidi vamizi nchini Iraq lakini imelezimika kuanza kuviondoa vikosi vyake nchini humo kutokana na mapambano ya wananchi au muqawama katika hali ambayo nchi kama vile Japan na Ujerumani zimeshindwa kuilazimu Marekani kufunga vituo vyake vikubwa vya kijeshi katika ardhi za nchi hizo.

آماده//شکست‌ هیمنه آمریکا و اسرائیل فقط از مکتب خمینی کبیر(ره) برمی‌آمد/ مقاومت؛ موازنه کننده قدرت

Swali: Je, kwa mtazamo wako,  Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yana ujumbe upi muhimu kwa ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa.

Jibu: Moja ya mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu katika dunia ya leo ni kurejea tena Uislamu halisi kama ulivvyoarifishwa na Mtume Muhammad SAW.  Huu ni Uislamu ambao pia uliarifishwa na mjukuu wa Mtume  Imam Hussein AS ambaye alisisitiza na kuonyesha kivitendo kuwa Waislamu hawapaswi kudhalilika na kusalimu amri mbele ya watawala wa kidikteta na wenye kiburi.  Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliweza kuibua mwamko wa Kiislamu ambapo leo Waislamu wengi wanaamini kuwa Uislamu una suluhisho kwa matatizo yote yaliyopo katika nchi za Kiislamu na duniani kote.

Swali:  Je, ni kwa nini nchi za Magharibi zinaishinikiza na kuiwekea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ni vipi fikra za Imam Khomeini zinaweza kutumiwa kukabiliana na njama hizo za madola ya kiistikbari?

Jibu: Ni kwali, Maadui wanapanga njama lakini ifahamike kuwa,  Mwenyezi Mungu naye pia anapanga Ila Mwenyezi Mungu ndio mbora wa mipango yote. Tizama matokeo ya vikwazo na mashinikizo, kinyume na walivyotarajia Mapinduzi ya Kiislamu yameimarika na yana uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto. Kufuatia misingi iliyowekwa na Imam Khoemini na kuimarishwa na Kiongozi Muadhamu Ayatullah Khamenei, leo Mapinduzi ya Kiislamu yananawiri zaidi.

Swali: Una jambo lolote la kuongeza katika mazungumzo haya?

Jibu: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuwa tunaishi katika zama za Mapinduzi Adhimu ya Kiislamu na sisi ni miongoni mwa vijana ambao walifunguliwa macho kuyaona mapinduzi haya na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi, fikra zake halisi za Uislamu ulioletwa na Mtume Muhammad SAW sambaba na ushujaa wake sawa na wa Imam Ali AS na mapambano yake ambayo ni sawa na mapambano ya Imam Hussein AS. Kufuatia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, maadui wamekuwa wakidhoofika kote duniani na nukta hii inaonyesha kuwa Mapinduzi ya Kiislani yanafungua njia ya kudhihiri Imam Mahadi, Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake.

3953121

captcha