IQNA

Rais Hassan Rouhani
15:43 - February 10, 2021
Habari ID: 3473639
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Kusimama kidete wanachi wa Iran na tadbiri ya serikali ni mambo ambayo yalipelekea serikali iliyopita ya Marekani kushindwa katika sera za vikwazo na mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo Jumatano alipohutubu kwa njia ya video katika sherehe za kuadhimisha mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Sambamba na kutoa salamu zake za kheri na fanaka kwa mnasaba huo, Rais Rouhani ameongeza kuwa: "Taifa kubwa la Iran lilisimama kidete mbele ya Donald Trump, mtawala dikteta aliyekuwa katika Ikulu ya White House. Kwa subira na mapambano wananchi wa Iran waliweza kumshinda mtawala huyo."

Rais Rouhani ameongeza kuwa, iwapo punde baada ya kuondoka Marekani katika mapatano ya JCPOA Iran nayo ingejiondoa katika mapatano hayo, njama ya Israel na Marekani ingedhihiri katika kurasa za historia."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekumbusha kuhusu vikwazo vya kidhalimu vya Marekani na mashinikizo ya juu kabisa ya utawala wa Trump dhidi ya Iran na kusema: "Watu wote wa dunia leo wana deni kubwa kwa taifa la Iran kwani mapambano ya Wiarani na tadbiri ya serikali ya Iran ndio chanzo cha kupata pigo serikali ya Trump."

Rouhani amesisitiza kuwa hakuna shaka kuhusu kuwa na taathira taifa na serikali ya Iran katika kuiangusha serikali ya kidikteta ya Trump na kuongeza kuwa, leo dunia ina usalama na inahisi kuwa sheria zinazingatiwa na uthabiti umerejea baada ya kuondoka Trump. Kwa msingi huo dunia ina deni kubwa kwa taifa la Iran.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikwazo, corona, mashinikizo ya vyombo vya habari na vita vya kisaikolojia na vitisho vya kijeshi ni vitisho vinne ambavyo Jamhuri ya Kiislamu imekabiliana navyo katika kipindi cha mwaka moja uliopita. Amesema pamoja na kuwepo vitisho hivyo vyote, taifa la Iran limesimama kidete. Ameongeza kuwa, ingawa zama za vikwazo vya juu kabisa na zama za vita vya kiuchumi zimefika ukingoni lakini taifa la Iran bado kunahitajika subira na muqawama hadi kufikia ushindi kamili.

Kuhusiana na shughuli za nyuklia za Iran, Rais Rouhani amesema: "Iwapo kundi la 5+1 litatekeleza ahadi zake, Iran nayo itafungamana na ahadi zake katika mapatano ya JCPOA. Amesema bila shaka taifa la Iran litafanikiwa kwa kutumia njia ya kisiasa na mazungumzo na dunia.

/3953335

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: