IQNA

Kiongozi Muadhamu wa mapinduzi ya Kiislamu

Uislamu unamheshimu mwanamke, Wamagharibi wanamtazama kama wenzo

19:05 - February 03, 2021
Habari ID: 3473616
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria tofauti za kimsingi za mtazamo wa Uislamu na ulimwengu wa Magharibi mwa mwanamke na kusema kuwa,Uislamu na Jamhuri ya Kiislamu vinamtazama mwanamke kwa jicho la heshima ilihali mtazamo ulionea Magharibi kuhusu mwanamke ni wa kumtazama kiumbe huyu kama bidhaa na wenzo.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo mjini Tehran katika kikao chake kwa njia ya mawasiliano ya Intaneti na wasomaji wa tungo za mashairi za kuwasifu Ahlul-Baiti AS ambapo sambamba na kutoa mkono wa kheri, baraka na fanaka kwa mnasaba wa kukumbuka maadhimisho ya kuzaliwa Bibi Fatma Zahra AS binti ya Mtume SAW, maadhimisho ya hadhi na daraja ya mwanamke na mama, kumbukuumbu ya kuzaliwa Imam Khomeini na vilevile sherehe za Alfajiri Kumi amesema kuwa, katika Uislamu mwanamke na mwanaume hawana tofauti yoyote katika suala la thamani za Kimwenyezi Mungu na kibinadamu, ingawa wana majukumu ya pamoja na maalum, na ni kwa sababu hiyo ndio maana Mwenyezi Mungu ameiumba miili yao kulingana na majukumu ya kila mmoja wao.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, Sisi tunajifakharisha na mtazamo wa Uislamu kuhusiana na mwanamke na wakati huo huo, tunalalamikia mtazamo mbaya wa ulimwengu wa Magharibi kwa mwanamke na mtindo wa maisha katika ulimwengu huo.

Ayatullah Ali Khamenei ameashiria propaganda za Wamagharibi kwamba, Uislamu na hijabu ya Kiislamu vinambinya mwanamke na kumzuia asionyeshe kipaji chake na kusema kuwa, huu ni uonngo wa wazi kabisa, na ushahidi wa kuthibitisha kutokuwa kweli madai  hayo ni wanawake katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kiongozi Muiadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, katika historia ya Iran hakuna wakati ambao walichomoza wanawake wasomi na wanaharakati katika nyuga mbalimbali za kijamii, kiutamaduni, kielimu, kisiasa, sanaa na kiuchumi kama ilivyo hii leo; na haya yote yamepatikana kwa baraka za Uislamu.

3951773

captcha