IQNA

22:57 - February 01, 2021
Habari ID: 3473610
TEHRAN (IQNA)- Wabunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) leo wamejadidisha kiapo cha utii kwa malengo ya Imam Khomeini, Mwenyezi Mungu Amrehemu, katika Haram ya muasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Akizungumza katika kikao hicho, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Imam Khomeini (MA) alihuisha tena Uislamu na izza na heshima ya Waislamu ulimwenguni.

Dakta Muhammad Baqir Qalibaf amesisitiza kuwa hatua ya Imam Khomeini ya kusimama kidete mkaba wa utawala dhalimu wa Kipahlavi, wanaopenda makuu, mabeberu na wakandamizaji duniani, ilipelekea kuhuisha tena Uislamu, izza na heshima ya Waislamu kote ulimwenguni.

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema pia kuwa Imam Khomeini alikuwa ni hakika na alituwekea mbele yetu maisha ya kweli na njia ya  wazi na ya kuhisika ya ulimwengu wa leo.

Miaka 42 iliyopita iliyosadifiana na tarehe Mosi Februari 1979, Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alirejea nchini Iran baada ya kuwa ubaidishoni kwa muda wa miaka 15.

Kurejea Imam Khomeini nchini Iran kuliharakisha kupatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu; kwai siku 10 baadaye yaani tarehe 11 Februari 1979, Mapinduzi ya Kiislmu yalipata ushindi na kuhitimisha utawala wa dikteta Shah. Sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran zinajulikana kwa jina maarufu la Bahman 22. Sherehe hizo mwaka huu zinafanyika tofauti ya miaka ya huko nyuma kutokana na maambukizi ya kirusi cha corona.

3951258

Kishikizo: iran ، imam khomeini ، bunge ، qalibaf
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: