IQNA

11:31 - March 12, 2021
News ID: 3473728
TEHRAN (IQNA)-Bunge la Umoja wa Ulaya limepasisha azimio ambalo limeitaka Bahrain isitishe mara moja ukandamizaji wa haki za binadamu za wanaharakati na wafungwa wa kiitikadi nchini humo.

Azimio hilo lilipitishwa kwa wingi wa kura Alhamisi ambapo wabunge 633 waliunga mkono 11 walipinga na 45 walijizuia kupiga kura.

Aidha azimio hilo limesema hali ya haki za binadamu inaendelea kuwa mbaya nchini Bahrain hasa baada ya ufalme huo kuanza kukabiliwa na mwamko wa wananchi wanaopinga ukandamizaji.

Wabunge hao wa Ulaya ameangazia kadhia ya wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa nchini Bahrain na kusema kuna dosari nyingi na katika kesi zao na uadilifu haujatendeka.

Mwamko wa watu wa Bahrain dhidi ya utawala wa kifalme ulianza Februari 14 mwaka 2011, na ungali unaendelea licha ya utawala huo dhalimu kushadidisha ukandamizaji na utumiaji mabavu dhidi ya wananchi hao wanaotaka mabadiliko.

Tokea Februari 14 mwaka 2011 hadi sasa utawala wa Aal Khalifa umewakamata na kuwafunga jela zaidi ya raia 11,000 kwa visingizio mbali mbali visivyo na maana. 

Malalamiko na maandamano hayo  ya wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala dhalimu wa nchi hiyo yalianza tarehe 14 Februri mwaka 2011. Mwanzoni walikuwa wakitaka kufanyika mabadiliko katika mfumo wa utawala wa nchi hiyo hasa kuondolewa ubaguzi, lakini taratibu maandamano hayo yalichukua sura mpya ya ghasia kufuatia hatua ya utawala wa Saudia ya kutuma askari wake katika nchi hiyo jirani kwa ajili ya kuwakandamiza wapinzani wa utawala wa Aal Khalifa. Utawala huo umekuwa ukitumia mbinu tofauti za kidikteta na za mkono wa chuma dhidi ya wapinzani ikiwa ni pamoja na kutolewa hukumu za kifo dhidi yao.

3474225

Tags: bahrain ، khalifa
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: