IQNA

Bahrain yakataa kulaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina

20:21 - March 25, 2021
Habari ID: 3473761
TEHRAN (IQNA) – Mwakilishi wa ufalme wa Bahrain katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa amejizuia kulaani ukiukaji wa haki za binadamu na ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina

Mwakilishi huyo wa serikali ya Bahrain kwa mara ya kwanza katika Ulimwengu wa Kiarabu hakuwa tayari kulipigia kura ya ndio azimio la Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa la kulaani hatua za utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina. 

Ripoti zinasema kuwa, Bahrain haikuhudhuria kikao hicho cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Msimamo huo wa Bahrain umewakasirisha wananchi wa Palestina hasa ikizingatiwa kuwa, aghalabu ya nchi za Ulaya zimelipigia kura ya ndio azimio hilo la kulaani ukiukaji wa haki za raia wa Palestina unaofanywa na Israel. 

Bahrain ni nchi ya kwanza ya Kiarabu kujiondoa katika muungano wa kulaani hujuma na vitendo vya ukiukaji wa haki za Wapalestina unaofanywa na utawala wa Kizayuni.

Pamoja na hayo, azimio hilo la Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepasishwa kwa kura za ndio 32 kati ya 47 za nchi wanachama.

Bahrain na Imarati tarehe 15 mwezi Septemba mwaka jana zilikutana katika ikulu ya Rais wa Marekani (White House) na kusaini makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel. 

3474298

captcha