IQNA

19:30 - April 03, 2021
News ID: 3473779
TEHRAN (IQNA) – Watu wa Bahrain wameandamana katika mji mkuu, Manama, Ijumaa jioni wakitaka wafungwa wa kisiasa waachiliwe huru.

Katika maandamano hayo yaliyopewa anuani ya “Ijumaa ya Ghadahabu ya Wafungwa” waandamanaji waliwalaani watawala wa Bahrain kwa kuendelea kuwashikilia wanaharakati na watetezi wa haki katika hali mbaya gerezani.

Aidha walitaka wafungwa hao waachiliwe huru kwa kuzingatia hali mbaya gerezani kutokana na janga la corona.

Siku ya Alhamisi, kiongozi mkuu wa Kiislamu nchini Bahrain Sheikh Isa Qassim alionya kuwa wafungwa wa kisiasa nchini humo wanakabiliwa na hatari ya mauti gerezani na hivyo ametaka waachiliwe huru mara moja.

Mwamako wa watu wa Bahrain dhidi ya utawala wa kifalme ulianza Februari 14 2011. Mwamko huu ni tofauti na harakati zingine za mwamko katika uliwengu wa Kiarabu ukiwemo mwamko uliopelekea kuangushwa Zine El Abidine Ben Ali wa Tunisia au Husni Mubarak wa Misri. Tofauti ya mwamko wa watu wa Bahrain ni kuwa, nchi hiyo inapakana na Saudi Arabia ambayo ni mpinzani na adui mkubwa zaidi wa mwamko na mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu.

Kwa msingi huo, mwezi mmoja baada ya kuanza mwamko wa Februari 14, utawala wa Saudia ulituma wanajeshi wake Bahrain kwa lengo la kuwakandamiza raia wa nchi hiyo. Askari hao vamizi wa Saudia waliingia Bahrain katika fremu ya 'Ngao ya Kisiwa' ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi. 'Ngao ya Kisiwa' ni mapatano ya ushirikiano wa kijeshi wa nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kwa lengo la kukabiliana na hujuma ya kigeni.

Hivi sasa ukiwa ni mwaka wa 10 tokea uanze mwamko wa watu wa Bahrain, wanajeshi wa Saudia na pia wale wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) bado wako nchini Bahrain na wanashirikiana na askari waliokodiwa wa utawala wa ukoo wa Aal Khalifa katika kuwakandamiza wananchi ambao wamekuwa wakiandamana kupigania mageuzi hasa ya kutaka kuwepo utawala unaochaguliwa moja kwa moja na wananchi.

 

آغاز تظاهرات «جمعه خشم» در بحرین + عکس
 
آغاز تظاهرات «جمعه خشم» در بحرین + عکس
 
آغاز تظاهرات «جمعه خشم» در بحرین + عکس
 
آغاز تظاهرات «جمعه خشم» در بحرین + عکس
 

  3962105

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: