IQNA

23:54 - August 27, 2020
Habari ID: 3473110
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Kishia huko Bahrain Ayatullah Isa Qassim amelaani utawala wa ufalme wa Al Khalifa nchini humo kwa kufunga misikiti ya Mashia katika mji wa Hamad na kusema hatua hiyo itaibua fitina.

Amesema uamuzi huo ni sawa na maamuzi ambayo kwa mtazamo wa umma yataibua fitina na kuvuruga mazungura ya msimu huu wa kukaribia Siku ya Ashura.

Ayatullah Isa Qassim amesema misikiti iliyofungwa ni ile ambayo huandaa Majlis za kukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS.

Amesema utawala wa ukoo wa Aal Khalifa unafaa kufahamu kuwa hatua kama hizo hazitawafanya waumini wausahau Uislamu na Imam Hussein AS.

Tokea mwaka 2011 hadi sasa utawala wa Aal Khalifa umetoa hukumu bandia 40 za kifo dhidi ya watu wanaolalamikia uongozi mbovu wa watawala ambao ni vibaraka wa Saudia na nchi za Magharibi. Mahakama ya Juu ya Bahrain imekuwa ikiwaelekezea wapinzani wa utawala huo tuhuma bandia kama vile kushambulia askari usalama au kupanga njama za kutekeleza operesheni za kigaidi na hatimaye kuwapa vifungo vya muda mrefu na kutoa hukumu za kifo dhidi yao.

Hukumu mbili zilizotolewa hivi karibuni dhidi ya vijana wawili wa nchi hiyo kwa kwa madai bandia kuwa waliwashambulia askari usalama pia zimetolewa kwa msingi huo huo. Hii ni katika hali ambayo vijana hao hawakuwa na kosa jingine ghairi ya kuukosoa utawala wa Manama kwa kuwakandamiza raia na kutozingatia matakwa yao.

 

3472392

Kishikizo: ashura ، isa qassim ، bahrain ، ashura
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: