IQNA

22:52 - March 16, 2021
News ID: 3473739
TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa kale wa Al-Aydarus katika mji wa Aden nchini Yemen ni kati ya misikiti ya kale mjini humo lakini sasa unakaribia kubomoka na kuangamia kutokana na kupuuzwa hasa katika kipindi hiki cha vita nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa katika tovuti ya Al Jazeera, Msikiti wa Al-Aydarus ambao ni msikiti wa Twariqa uko juu ya mlima katika eneo la Crater (Kraytar) palipo kijiji cha kale zaidi mjini Aden.

Msikiti huo wenye kuta nyeupe na kuba la aina yake ulijengwa miaka zaidi ya 500 iliyopita yaani mwaka 1484 MILADIA au 899 Hijria Qamaria..

Msikiti huo ulipewa jina la Sheikh Abu Bakr Al-Aydarus aliyekuwa Walii na mwanazuoni maarufu wa Kiislamu wa Aden.  Sheikh Abu Bakr Al-Aydarus ambaye alikuwa akifunza Uislamu ndiye aliyeanzisha ujenzi wa msikiti huo na baada ya kufariki alizikwa pembizoni mwa msikiti huo.

Usanifu majengo wa msikiti huo unaonekana kuiga mtindo wa ujenzi wa misikiti nchini India.

Msikiti wa Al-Aydarus ulikarabatiwa mwaka 1859 na wakati wa vita vya Yemen mwaka 1994 uliharibiwa na watu wenye misimamo mikali ya kidini.

Picha za msikiti huo zilitumiwa katika baadhi ya stempu za posta mjini Aden mwaka 1938.

Hivi karibuni taasisi za kimataifa zimetoa  wito wa kukarabatiwa msikiti huo wa kale kwani unakaribia kubomoka kutokana na uharibifu katika  zama mbali mbali za kivita.

Hizi hapa chini ni baadhi ya picha za msikiti wa Al-Aydarus mjini Aden, Yemen

 
 
مسجد باستانی «العیدروس» عدن در آستانه تخریب

مسجد باستانی «العیدروس» عدن در آستانه تخریب
 
ا

3959862

Tags: yemen ، al aydarus ، msikiti
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: