IQNA

Nakala 700,000 za Qur'ani zasambazwa miongoni mwa wanafunzi wa Kiislamu Afrika

13:52 - March 30, 2021
Habari ID: 3473770
TEHRAN (IQNA)- Shirika moja la misaada ya Uturuki limesambaza nakala zaidi ya 700,000 za Qur'ani Tukufu kwa wanafunzi wa vyuo vya Kiislamu barani Afrika.

Ali Othman Aslanchi, mwakilishi wa Jumuiya ya Khayrat ya Uturuki katika mkoa wa Izmir nchini Uturuki amesema usambazwaji wa nakala hizo za Qur'ani ulianza mwaka 2017.

Amesema walichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa Waislamu wengi Afrika walio katika vyuo vya kidini hawana nakala za kutosha za Qur'ani Tukufu.

Aidha amesema tokea mwaka 2017 wamesambaza misahafu 723,000 za Qur'ani barani Afrika. Amesema nchi za Niger na Burkina Faso kwa pamoja zimepata misahafu 126,000 na hivyo zimepokea idadi kubwa zaidi ya misahafu hiyo.

3961701

Kishikizo: uturuki afrika misahafu
captcha