IQNA

18:52 - April 17, 2021
News ID: 3473823
TEHRAN (IQNA) – Qarii maarufu wa Qur’ani Tukufu nchini Misri ametuma ujumbe kwa Waislamu kote duniani kwa mnasaba wa kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika ujumbe huo amemuomba Mwenyezi Mungu SWT awatakabalie Waislamu Saumu yao katika mwezi huu mtukufu.. Baada ya hapo amesoma aya 185 ya Sura al Baqarah katika Qur’ani Tukufu isemayo: “ Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.”

Sheikh Taruti alizwaliwa mwaka 1965 katika kijiji cha Tarut karibu na mji wa Zagazig jimboni Sharqia. Alianza kuhifadhi Qur’ani akiwa na umri wa miaka mitatu na alifanikiwa kuhifadhi Qur’ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka 8. Taruti alisoma katika tawi la Zagazig la Chuo Kikuu cha Al Azhar na aliendelea  kuimarisha uwezo wake wa Qur’ani kwa kupata mafunzo kwa kutoka kwa wasomi wakubwa kama vile Sheikh Mohammad Al-Lithi, Shahat Anwar na Saeed Abdul Samad.

3964620

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: