IQNA

19:25 - April 21, 2021
News ID: 3473837
TEHRAN (IQNA)- Rais Muhamadu Buhari huhudhuria darsa za tafsiri ya Qur'ani Tukufu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa taarifa, siku ya Jumanne, Rais Buhari alijunga na Waislamu katika Msikiti wa Ikulu ya Rais mjini Abuja ambapo amefuatilia darsa ya tafsiri ya Qur'ani Tukufu.

Rais Buhari ambaye alikuwa ameandamana na washauri wake alikuwa akihudhuria darsa hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili kutokana na kuwa msikiti huo ulifungwa wakati wote wa mwezi wa Ramadhani mwaka jana ili kuzuia kuenea virusi vya COVID-19.

Rais wa Nigeria amesema janga la COVID-19 ni 'mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu".

Imamu wa msikiti huo ametoa wito kwa watu wa Nigeria kuendelea kuzingatia kanuni za kuzuia kuenea COVID-19.

/3474515

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: