TEHRAN (IQNA)- Kwa mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao Qur’ani Tukufu imeteremshwa, Maktaba ya Kitaifa ya Qatar imeandaa maonyesho ya “Maandishi ya Qur’ani Tukufu Katika Karne Zilizopita.”

Maonyesho hayo ambayo yanafanyika katika fremu ya program za ‘Doha Mji Mkuu wa Utamaduni wa Ulimwengu wa Kiislamu Mwaka 2021’, yamejumisha kaligrafia katika maandishi ya Qur’ani, sanaa iliyotumika kupamba misahafu n.k.
Katika kipindi chote cha historia, Waislamu wamejitahidi kutunza na kuzingatia Qur’ani Tukufu kwa njia mbali mbali na moja ya njia hizo ni katika kuandika misahafu kwa kaligrafia.