IQNA

Israel yaua raia 133 Wapalestina, wakiwemo sita wa familia moja

19:33 - May 15, 2021
Habari ID: 3473913
TEHRAN (IQNA)-Raia Wapalestina 133, wakiwemo sita wa familia moja, wameuawa katika mashambulio ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza.

Taarifa zinasema Utawala wa Kizayuni unaendelea kufanya jinai za kinyama na za kutisha dhidi ya Wapalestina. Habari za karibuni kabisa zinasema kwamba utawala huo katili umeua kwa umati familia ya watu saba magharibi mwa mji wa Ghaza katika shambulio lake la anga. Watu hao waliouliwa kikatili na Wazayuni ni wanawake watano na watoto wadogo wawili

Kwa mujibu wa taarifa, alfajiri ya leo Jumamosi, ndege za kivita za Israel zimeshambulia nyumba ya raia mmoja wa Palestina aitwaye Abu Hatab katika kambi ya wakimbizi wa al Shati na kuua kwa umati watu 7 wa familia moja.

Duru nyingine za Palestina zimetangaza habari ya kushambuliwa boti za Wapalestina na jeshi la utawala wa Kizayuni.

Habari za karibuni kabisa zinasema kuwa, utawala dhalimu wa Israel Wapalestina 126 wameshauawa wakiwemo watoto 38 na wanawake 20  tokea utawala huo unazisha vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza Jumatatu. Wapalestina wengine zaidi ya 1000 wameshajeruhiwa hadi hivi sasa.

Wakati huo huo, Brigedi za Izzuddin al Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimefyatua makumi ya makombora kulenga mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Tel Aviv na wa bandari wa Ashdod kujibu jinai ya mauaji ya halaiki yaliyofanywa na jeshi la utawala huo haramu katika kambi ya wakimbizi wa Kiplaestina ya Shat'i.

Ashdod ndio bandari kubwa zaidi ya utawala ghasibu wa Israel ambapo zaidi ya asilimia 60 ya bidhaa za Wazayuni zinaingizwa kupitia bandari hiyo. Makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina hadi sasa yamevurumisha mamia ya makombora ambayo yamelenga Israel na kusababisha hasara kubwa.

Utawala ghasibu wa Israel ulianzisha uvamizi dhidi ya Ghaza baada ya Wapalestina katika eneo hilo kuandamana kulalamikia vikali ukandamizaji wa Israel dhidi ya Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem). Kitendo cha askari katili wa Israel kuuvamia Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds na kuwahujumu Wapalestina waliokuwa wakiswali katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kimehesabiwa kuwa ni kuvuka mstari mwekundu wa Wapalestina na Waislamu duniani.

Katika kujibu jinai hizo za Israel makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza yamevurumisha mamia ya makombora katika miji ya Israel ukiwemo mji mkuu Tel Aviv na kusababisha hasara kubwa. Waisraeli  wasiopungua 7 wameangamizwa katika oparesheni hizo za ulipizaji kisassi za Wapalestina. 

3474715

Kishikizo: palestina ، ghaza ، jinai ، israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :