IQNA

Watetezi wa Palestina

Waislamu Kanada: Trudeau aunge mkono uchunguzi wa uhalifu wa Kivita wa Israel katika ICJ

15:45 - January 10, 2024
Habari ID: 3478177
IQNA - Mashirika kadhaa ya Kiislamu nchini Kanada (Canada) yamemuomba Waziri Mkuu Justin Trudeau kuunga mkono uchunguzi wa kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita wa utawala wa Israel huko Gaza.

Ombi hilo lilitolewa katika barua ya wazi iliyosainiwa na asasi za kiraia na jumuiya 250 za Kanada chini ya Baraza la Taifa la Waislamu wa Kanada (NCCM).

Barua hiyo inaitaka Kanada kuunga mkono kesi ya Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu jinai za mauaji ya kimbari za utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

"Kanada lazima iunge mkono uchunguzi usio na upendeleo wa uhalifu wa kivita unaowezekana kufanywa huko Gaza," NCCM ilisema kwenye chapisho kwenye X.

"Kanada lazima iunge mkono uwajibikaji na haki. Ni wakati wa kutambua mamlaka ya ICJ katika suala hili," iliongeza

Nchi zaidi zimeungana na Afrika Kusini katika kesi iliyowasilishwa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu vita vya mauaji ya kimbari vya utawala huo kwenye dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.


Maldives, Namibia na Pakistan zimetangaza kuunga mkono kesi ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Tel Aviv wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne.

Afrika Kusini ilifungua kesi dhidi ya Israel mwishoni mwa mwezi Disemba, baada ya takriban miezi mitatu ya vita vya maangamizi ya umati vya Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Kesi hiyo ilisema hatua za Israel ni "mauaji ya kimbari kwa sababu zina nia ya kuleta uharibifu wa sehemu kubwa ya kundi la taifa, rangi na kaumu ya Palestina."

Ombi hilo pia lilisema mashambulizi ya Israel yanakiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari ya Umoja wa Mataifa, na kuitaka mahakama hiyo "iamuru Israel isitishe mauaji na madhara makubwa ya kiakili na kimwili kwa Wapalestina huko Gaza."

Nchi nyingine ambazo tayari zimeonyesha kuunga mkono kesi hiyo ni pamoja na Bolivia, Jordan, Malaysia na Uturuki. ICJ itaanza kusikiliza kesi hiyo Alhamisi na Ijumaa wiki hii.

Israel ilianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina  kwenye Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba baada ya Hamas kutekeleza operesheni ambayo haijawahi kushuhudiwa dhidi ya utawala huo wa Kizayuni ikiwa ni kulipiza kisasi kwa ukatili wa utawala huo  dhidi ya watu wa Palestina.

Hadi sasa utawala wa Israel imewauwa Wapalestina wasiopungua 23,300 wengi wao wakiwa wanawake na watoto na kuwajeruhi wengine 59,000. Maelfu zaidi pia wametoweka na wanaodhaniwa wamekufa chini ya vifusi katika Ukanda wa Gaza, ambao umezingirwa kikamilifu na Israel.

3486758

Habari zinazohusiana
captcha