IQNA

Picha za maeneo ya Israel ambayo yameharibiwa kwa makombora ya Hamas

19:59 - May 14, 2021
Habari ID: 3473909
TEHRAN (IQNA)- Tawi la kijeshi la Harakati ya Mapamabno ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) limevurumisha mamia ya makombora katika miji ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kusababisha hasara kubwa.

Katika hatua ya kulipiza kisasi jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel,  Brigedi za Ezzedin Qassam Tawi la Kijeshi la Hamas imevurumisha makombora ndani ya miji ya Israel kusababisha hasara kubwa mbali na kuangamiza Wazayuni 9.

Hizi hapa ni picha maalumu tulizopokea kuhusu hasara waliyopata Wazayuni.

تصاویر اختصاصی گردان‌های قسام از خسارات موشکی در فلسطین اشغالی
 
Hadi sasa Wapalestina 119, wakiwemo watoto 28, wameuawa shahidi tokea Jumatatu wakati utawala wa Kizayuni wa Israel ulipoanzisha mashambulizi dhidi ya Ghaza huku wengine 600 wakiwa wamejeruhiwa.

Utawala ghasibu wa Israel ulianzisha uvamizi dhidi ya Ghaza baada ya Wapalestina katika eneo hilo kuandamana kulalamikia vikali ukandamizaji wa Israel dhidi ya Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem). Kitendo cha askari katili wa Israel kuuvamia Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds na kuwahujumu Wapalestina waliokuwa wakiswali katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kimehesabiwa kuwa ni kuvuka mstari mwekundu wa Wapalestina na Waislamu duniani.

Katika kujibu jinai hizo za Israel makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza yamevurumisha mamia ya makombora katika miji ya Israel ukiwemo mji mkuu Tel Aviv na kusababisha hasara kubwa. Waisraeli  wasiopungua 9 wameangamizwa katika oparesheni hizo za ulipizaji kisassi za Wapalestina. 

3971495/

Kishikizo: palestina ، quds tukufu ، vita ، wazayuni ، israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :