IQNA

12:50 - July 14, 2021
News ID: 3474099
TEHRAN (IQNA)- Iran na Marekani hatimaye zitafikia mapatano ya nyuklia, amesema mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha George Washington.

Katika mahojiano na IQNA Michael Barnett amesema: “Nadhani utawala wa Biden unataka mapatano na Iran ambayo yatakuwa bora Zaidi ya yale yaliyofikiwa wakati wa Obama. Iran nayo pia inataka mapatano bora.”

Aidha amesema anatabiri kuwa pande hizo mbili hatimaye zitafikia mapatano na kuongozwa kuwa kile kinachoweza kuzuia mapatano ni tukio la uchokozi.

Hivi karibuni, mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema sasa wakati umewadia kwa Marekani na nchi tatu za Ulaya kuchukua maamuzi magumu kwa ajili ya kuanza kufungamana tena kikamilifu na mapatano ya kimataifa ya nyuklia, JCPOA.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Usalama kilichoandaliwa kwa ajili ya kuchunguza ripoti za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu JCPOA na utekelezaji wa azimio nambari 2231 la baraza hilo, Majid Takht Ravanchi amesema Iran imethibitisha kivitendo ukweli wake iwe ni katika kipindi cha kufanyika mazungumzo ya JCPOA au wakati wa kutiwa saini na kutekelezwa mapatano hayo muhimu ya kimataifa. Mazungumzo ya kuhuisha mapatano hayo yamekuwa yakiendelea kwa miezi kadhaa sasa katika mji wa Vienna nchini Austria.

Kuhusiana na kuondoka wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Afghanistan, amesema askari wa Marekani walibakia katika nchi hiyo kwa muda wa miaka 20 bila mafanikio yoyote.

Akiashiria hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel, amesema nchi za Kiarabu zilizochukua hatua hiyo tokea mwanzo hazikuwa zinaunga mkono ukombozi wa Palestina.

Aidha amesema utawala wa Biden utaendeleza sera za huko za Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

/3475227/

Tags: marekani ، nyuklia ، kiarabu ، iran
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: