Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, nafasi ya kwanza katika mashindano hayo ya qiraa ya Qur’ani Tukufu imechukuliwa na Abdullah Karbalai wa Iraq ambaye amefuatiwa na Mohammad Ali Qassim wa Lebanon huku nafasi ya tatu akiwa ameshika Majid Ananpour wa Iran.
Jumuiya ya Qur’ani ya Irshad wa Tawjih ya Lebanon inapata himaya ya Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah na imeandaa mashindano hayo ya Qur’ani kwa njia ya intaneti.
Mashindano hayo yalianza Jumamosi 10 Julai na washindi wammetangazwa leo Ijumaa.
Wasomaji Qur’ani 322 kutoka nchi 40 duniani wameshiriki katika duru za mchujo za mashindano hayo na hatimaye washiriki 10 bora wametangazwa.