Mashindano haya yalifanyika kwa njia ya mtandaoni wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, na yalivutia ushiriki wa Maqari wa Qur'ani 150 kutoka nchi mbalimbali.
Wito wa kushiriki ulitangazwa kabla ya Ramadhani na maqari waliombwa kuwasilisha video za usomaji wao wa aya maalum zilizopangwa.
Katika awamu ya mwanzo, zaidi ya Maqari150 waliwasilisha kazi zao. Kati ya kundi hilo, 36 walichaguliwa kuingia raundi ya mchujo.
Majaji waliangalia video hizo na kupunguza idadi hadi washiriki 13 wa nusu fainali. Kila mmoja aliombwa kutuma video mpya ya usomaji wa aya zilizotengwa, na sita kati yao walichaguliwa kufika katika raundi ya fainali.
Washiriki wa fainali walikuwa ni Majid Ananpour kutoka Iran, Bilal Hamwi kutoka Uturuki, Ezzat Al-Sayyid Rashid kutoka Misri, Sediq Yaseen Hosseini kutoka Afghanistan, Ahmed Razzaq Al-Dalfi kutoka Iraq, na Wudan Hermoko kutoka Indonesia.
Majid Ananpour kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitunukiwa tuzo ya juu kabisa katika mashindano haya.
3492768