Idul-Adhha, yaani Sikukuu ya Kuchinja ni miongoni mwa Sikukuu kubwa za Waislamu.
Katika siku hii tukufu, Mahujaji waliokwenda kuzuru Nyumba ya Mwenyezi Mungu huchinja kwa amri ya Mola na kwa ajili ya kupata radhi zake; na kwa kufanya hivyo, huendeleza na kuenzi kumbukumbu ya Mtume mteule wa Allah, Nabii Ibrahim (AS).
Zifuatazo ni picha za siku kuu ya Idi katika maeneo mbali mbali mbali duniani.
Wanawake wa Palestina wanapiga picha wakiwa katika Msikiti wa Al-Aqsa kwa ajili ya Sala ya Idul Adha
Waislamu Iraq katika Sala ya Idul Adha prayers barabarani nje ya msikiti wa Abu Hanifa mosque katika mtaa wa Adhamiya mjini Baghadad
Watoto wakicheza baada ya Sala ya Idul Adha katika Msikiti al-Azhar mjini Cairo, Misri.
Mtoto akiwa amesimama miongoni mwa waumini katika Sala ya Idul Adha mjini Sanaa, Yemen.
Waislamu baada ya Sala ya Idul Adha katika Msikiti wa Tahsin Sorani huko Kirkuk, Iraq.
Waumini katika Sala ya Idul Adha katika Uwanja wa Medani ya al-Farah huko Khartoum, Sudan.
Waislamu katika Sala ya Idul Adha katika Msikiti wa Lhokseumawe, mkoani Aceh , Indonesia.
Waumini katika Sala ya Idul Adha katika Msikiti Mkuu Camlica huko Istanbul, Uturuki
Watoto wakiwasili katika msikiti kwa ajili ya Sala ya Idul Adha huko Herat, Afghanistan.
Furaha baada ya Sala ya Idul Adha prayers katika Uwanja Dinamo huko Bucharest, Romania.
Wanawake Waislamu wakiwa katika Sala ya Idul Adha Nairobi, Kenya.