IQNA

Waislamu wa Marekani kuadhimisha Idul Adha Ijumaa Juni 6

19:04 - May 30, 2025
Habari ID: 3480761
IQNA-Kwa mujibu wa taarifa, mnamo Ijumaa, Juni 6, Waislamu wa Marekani wanapanga kuadhimisha mwanzo wa sikukuu hii inayohitimisha ibada ya Hija kwa kuswali pamoja na kusherehekea katika maeneo mbalimbali nchini humo. 

Idul Adha ambayo mara nyingi hutajwa kwa kifupi kama "Idi," inaadhimisha utii wa Nabii Ibrahim kwa Mwenyezi Mungu, alipokuwa tayari kumtoa kafara mwanawe Ismail kulingana na amri ya Mwenyezi Mungu. Sikukuu hii huadhimishwa kwa ibada za sala, zawadi ndogo kwa watoto, kuchinja na kisha kugawa nyama kwa familia na wasiojiweza, na mikusanyiko ya kijamii. Katika kipindi hiki, Waislamu hubadilishana salamu za "Idi Mubarak", ambazo humaanisha Eid yenye baraka.

KUMBUKA: Kwa Mahujaji walio katika mji mtakaftifu wa Makka, ibada za Hija huendelea kwa muda baada ya sala za Idul Adha. Ikumbukwe kuwa Idul Fitr, inayokuja baada ya mwezi mzima wa kufunga Ramadhani, ni sikukuu nyingine kubwa ambayo Waislamu huiadhimisha kila mwaka.

📅 Lini? Ijumaa, Juni 6. Sala ya Idi itaswaliwa asubuhi, na jamii nyingi huandaa sherehe za Idi kwa familia kwa siku nzima.

📍 Wapi? Sala na sherehe za Idi hufanyika katika misikiti ya mtaa au kwenye maeneo ya umma yaliyoandaliwa kwa mikusanyiko mikubwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na matawi ya Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani, (CAIR) au mashirika mengine ya Kiislamu kuhusu ratiba za Idi.

📸 Fursa ya Picha: Kila mwaka katika Idul Adha,  familia za Waislamu wa Marekani hukusanyika kwa sala na sherehe. Maeneo mengi ya ibada huandaa shughuli za watoto. Sala zenyewe zinavutia sana, kwani waumini hupangwa kwa mistari na kusujudu kwa pamoja. Washiriki hubadilishana mikumbatio baada ya sala kumalizika.

Katika Qur’an, kitabu kitakatifu cha Uislamu, Mwenyezi Mungu anasema: "Hivi ndivyo tulivyomweka Ibrahim mahali pa Nyumba (ya Ka’aba) tukimwambia: ‘Usimshirikishe yeyote nami, na itakase Nyumba yangu kwa wale wanaoizunguka, wanaosimama humo wakiswali, na wale wanaoinama na kusujudu. Tangaza Hajj kwa watu: watakujia kwa miguu na kwenye kila mnyama dhaifu; watafika kutoka kila bonde refu, kushuhudia manufaa yao na kulitaja jina la Mwenyezi Mungu katika siku zilizowekwa.” 📖 (Surah Al-Hajj, Aya 26-28)

Hija ni moja ya nguzo kuu tano za Uislamu. (Nguzo zingine ni: Shahada—kukiri imani, Swala—sala za kila siku, Zaka—kutoa sadaka mara kwa mara, na Saumu—kufunga katika mwezi wa Ramadhani.) Hija ni wajibu wa mara moja maishani kwa wale walio na uwezo wa kimwili na kifedha kufanikisha safari hiyo.

Baada ya Mahujaji kukamilisha sehemu kuu ya ibada ya Hija, Waislamu duniani kote hukusanyika kwa sala za kijumuiya siku ya kwanza ya Idul Adha sikukuu ya pili kati ya sikukuu kubwa mbili za Kiislamu.

3493269/

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: marekani idul adha
captcha